Saturday, January 18, 2025
HomeBusiness NewsORODHA YA WASANII KUMI BORA WANAOWANIA TUZO ZA AFRIMA USA AFRIKA

ORODHA YA WASANII KUMI BORA WANAOWANIA TUZO ZA AFRIMA USA AFRIKA

Katika ulingo wa sanaa ya Muziki hapa Afrika , wasanii wengi wameonyesha jitihada katika kazi zao za muziki. Baadhi wamechaguliwa katika tuzo za AFRIMA zitakazofanyika USA mwezi disemba. Baadhi ya wasanii kumi bora waliochaguliwa ni wafwatao

1.Diamond Platnumz

Diamond platnumz ni msanii bora Afrika Mashariki na kati. Yupo miongoni mwa wale waliotengwa kuwakilisha Afrika katika mashindano nchini USA. Simba kama vile anavyofahamika ndiye anayemiliki Record Label ya WCB Wasafi kule DAr es salam Tanzania, mojawapo ya Label tajika katika kurekodi mziki hapa Afrika kote. Nyimbo yake iliyovuma sana na ambayo ina watazamaji wengi katika mtandao wa YouTube ni “Yope” aliyomshirikisha msanii Inoss B kutokea nchini DRC.

2.Davido

Davido pia ni miongoni mwa wasanii bora walioteuliwa. Inatambulika kuwa nchini Nigeria yeye ndiye msanii tajika na mwenye mali mengi sana.Hivi majuzi mwanawe wa kike Davido na mkewe Chioma aliweza kuaga dunia na kisa cha kifo bado hakijatambulika bayana.

3.Tiwa Savage

Katika Afrika , Tiwa Savage ni miongoni mwa wasanii bora wanaoeka bidii katika sanaa ya muziki. Tiwa ana wafuasi wengi kutokea nchi yake kule Nigeria na pia mashabiki hakiki katika kati na mashariki mwa Afrika. siku chache alitembelea taifa la Kenya kwa muonekano na salamu kwa mashabiki wake.

4.Yemi Alade.

Pia ni miongoni mwa wanawake bora wanaofanya vyema katika muziki Africa.

5.Fireboy dml

Fireboy pia ni msanii kutoke nchi ya Nigeria . Ameteuliwa kwa baadhi ya watakaowakilisha Afrika kwa tuzo za AFRIMA. Nyimbo yake kali inayovuma kwa sasa ni Bandana ambayo ina zaidi ya watazamaji milioni 10 katika mtandao wa YouTube.

6.Wizkid

Naye pia ni msanii kutokea Nigeria. Anaonekana wa pili katika ulingo wa muziki na mwenye mali mengi baada ya Davido. Amewashirikisha baadhi ya wasanii wakubwa kutoka nchi za kigeni na hapa Afrika.

7.Burnaboy

Wasanii na wanamuziku kutoka Nigeria wanaonekana kuwa wengi mno kwenye orodha hii ya wasanii bora. Burnaboy alias the african giant kama anavyijiita pia yupo miongoni mwa wasanii walioteuliwa. Naye aidha muziki wake unaenziwa mno na mashabiki hivyo kumfanya kuwa msanii mashuhuri sana kote duniani.

8.Aya Starr

Vilevile pia ni msanii aliye na kijapi cha kuimba muziki wa afropop music . Sasa hivi ana ngoma ya Rush iliyopokelewa vyema na inaendelea kufanya vyema katika mitandao yote.

9.Ckay

Naye pia ameteuliwa na sanaa ya mashindano pale USA kama baadhi ya msanii bora wa mwaka.

10.Shenseea

Vile vile pia yupo miongoni mwa wasanii boya wa mwaka walioteuliwa katika mashindano ya tuzo ya Afriam. Hawa ndio wasanii waliochaguliwa Afrika kama best Artist of the Year. Hivi mashabiki kule ndio watakaoamua katika hawa wasanii kumi naye atakayekuwa mbabe na gwiji katika muziki hapa Afrika.

Dangote Dan Okoti
Dangote Dan Okotihttps://mtamaduni.co.ke
Dangote Dan Okotiia is a passionate blogger writing about trending news, celebrity news & gossip, technology, politics, business, sports, and all trending topics.
RELATED ARTICLES
- Advertisment -

Latest Posts